Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga Juni jana 13, 2023 mkoani Tabora wakati wa ufungaji wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ambapo alisema Rasimu ya Sera ya Elimu una mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 ukurasa 39 imeweka bayana Utambuzi na uendelezaji wa vipaji na vipawa katika elimu na mafunzo.
Kipanga, aliongeza kuwa fani ya michezo, sanaa na ubunifu duniani inatiliwa mkazo kwa kuwa kitaalamu ndiyo inayojenga na kuimarisha ufahamu na afya ya mwanadamu pamoja na kwamba michezo inaburudisha, inakuza uwezo wa kufikiri kwa namna nyingi.
"Serikali inatambua faida nyingi zinazopatikana kutokana na michezo zikiwemo kuimarisha stadi za kujifunza, kujenga na kuimarisha afya, kujenga nidhamu ya raia, kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya raia.
Vijana katika nchi mbalimbali wamekuwa wakijipatia kipato kutokana na michezo na sanaa, jambo ambalo imechangia kukuza uchumi wa nchi" amesisitiza Kiongozi huyo.










