Samia aialika Yanga Ikulu

04Jun 2023
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Samia aialika Yanga Ikulu

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameialika Timu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) Ikulu jijini Dar es Salaam kesho kupata chakula cha jioni, kwa ajili ya kuiponegza kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika iliyohitimishwa jana nchini Algeria.

 Taarifa hiyo ya mwaliko imetolewa leo (Juni 4,2023) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ambaye amesema Rais Samia amewapongeza Yanga kwa kucheza vizuri katika mchezo wa pili wa fainali hapo jana kwa kuwafunga wenyeji wa mchezo huo bao 1-0.

Amesema baada ya kuwafunga  Yanga ilijizoelea matokeo ya jumla ya mabao 2-2 japokuwa hawakufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Aidha, Msigwa amebainisha kuwa pamoja na kutotwaa ubingwa, Rais Samia anatambua kuwa Yanga wameipa heshima kubwa Tanzania.

Pia amewapongeza na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.