Taarifa iliyotolewa jana na Bodi ya Ligi chini ya Idara ya Habari na Mawasiliano, imesema sambamba na mabadiliko ya raundi hiyo ya 30, pia raundi ya 29 nayo imepangwa kucheza Juni 6, mwaka huu, badala ya Mei 24 kama ilivyopangwa awali.Bodi imesema imelazimika kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa klabu ya Yanga kucheza michezo yake mwili ya fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Mei 28 hapa nyumbani na Juni 3 nchini Algeria dhidi ya USM Alger.Imesema imeamua kufanya mabadiliko hayo baada ya majadiliano ya ndani yanayojikita kuhakikisha uwepo wa haki na usawa michezoni na kuondoa uwezekano wa upangwaji wa matokeo kama wataachia timu zingine ziendelee kucheza na zingine zisubiri."Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) inawataarifu kuwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu msimu wa 2022/23 zitacheza michezo yao ya mwisho raundi ya 30, Juni 9, mwaka huu ili kutoa nafasi kwa Yanga kucheza michezo yake ya fainali ya Kombe la Shirikisho,” ilisema sehamu ya taarifa hiyo ya Bodi.Kwa mujibu wa ratiba iliyotumwa kwa klabu hivi karibuni na kutangazwa kwa umma jana (juzi), michezo ya mwisho ya timu zote ukiondoa Yanga dhidi ya Prisons ilipangwa kufanyika Mei 28, lakini Bodi imelazimika kufanya mabadiliko hayo ili kuhakikisha uwepo na haki na usawa michezoni kuondoa mazingira ya upangaji wa matokeo.
Kwa mantiki hiyo, msimu wa Ligi Kuu 2022/2023 utafikia tamati Juni 9 kwa michezo hiyo ya mwisho.









