Klabu tano zilizoshinda Uefa mara nyingi zaidi

22May 2023
Na Mwandishi Wetu
UINGEREZA
Nipashe
Klabu tano zilizoshinda Uefa mara nyingi zaidi

LIGI ya Mabingwa Ulaya ni njia ‘takatifu’ kwa wachezaji na makocha mashuhuri barani Ulaya.

Mashindano hayo yanayojulikana kama Kombe la Uefa yanayotumia mtindo wa mtoano yanaunda kumbukumbu zisizosahaulika na kwa wale waliobahatika kubeba kombe.

Lakini ni klabu gani zimefurahia mafanikio zaidi kwenye michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya Klabu barani Ulaya?

Makala haya yanakuchambulia klabu tano zilizotwaa mara nyingi zaidi taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Real Madrid - 14

Kwa mara ya kwanza: 1956

Kwa mara ya mwisho: 2022

Ukweli wa kufurahisha: Real Madrid ndio inayoshikilia rekodi ya kushinda taji hilo mara nyingi mfululizo kwa mara tano (mwaka 1956 hadi 1960).

Los Blancos hao bila shaka wanatakiwa kupewa heshima ya kuwa timu iliyofanikiwa zaidi katika historia ya shindano hilo.

Klabu hiyo ya Hispania imetoa nyakati za kufurahisha zaidi kwenye mashindano hayo ya Ulaya, haswa bao la ushindi la Zinedine Zidane, ambalo liliipata taji la tisa klabu hiyo mwaka 2002.

Gareth Bale pia alifunga bao la kukumbukwa la tiktaka katika ushindi wao wa mwaka 2018, akiachia mkwaju wa juu kwa juu uliompita golikipa wa Liverpool, Loris Karius.

AC Milan - 7

Kwa mara ya kwanza: 1963

Kwa mara ya mwisho: 2007

Ukweli wa kufurahisha: AC Milan ilikuwa timu ya kwanza ya Italia kushinda Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1963.

Labda ushindi wa kukumbukwa zaidi wa Milan kwenye Ligi ya Mabingwa ulikuja mwaka wa 2007, waliposhinda kizingiti cha kiakili cha kuishinda Liverpool katika marudio ya fainali ya mwaka 2005.

Filippo Inzaghi alifunga mabao mawili mjini Athens na kukamilisha ushindi wa 2-1 huku wachezaji kama Kaka, Clarence Seedorf na Paolo Maldini wakiwa nyota kwenye mchezo huo.

Mapema katika muongo huo, Andriy Shevchenko alicheza vyema katika fainali ya mwaka 2003 ambapo ilizikutanisha klabu pekee za Italia, Milan dhidi ya Juventus. Raia huyo wa Ukraine alifunga mkwaju wa penalti ya ushindi pale kwenye dimba la Old Trafford nchini England na kuipa Milan taji la sita.

Bayern Munich - 6

Kwa mara ya kwanza: 1974

Kwa mara ya mwisho: 2020

Ukweli wa kufurahisha: Ushindi wa Bayern Munich wa 1974 ulikuwa wa kwanza na kwa mara ya kwanza na kipekee fainali kuamuliwa kwa mechi ya marudiano.

Baada ya sare ya 1-1 mjini Brussels dhidi ya Atletico Madrid, Franz Beckenbauer alinyanyua kombe siku mbili baadaye kutokana na ushindi wa 4-0.

Hakuna kitu kitamu kama kuwashinda wapinzani wako kwenye hatua kubwa zaidi na Bayern Munich walifanya hivyo walipoishinda Borussia Dortmund mnamo mwaka 2013, kwa hisani ya bao la dakika ya mwisho kutoka kwa Arjen Robben.

Mnamo 2001, Bayern ilishinda Valencia katika mchezo uliojaa mikwaju ya penalti. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1 huku timu zote zikifunga goli lakini ni Bayern walioibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti na kufanikiwa kutwaa taji lao la nne.

Mapema mwaka 2020 ilishuhudia Bayern wakitwaa taji lao la sita, wakiishinda Paris Saint-Germain katika fainali pekee iliyochezwa bila mashabiki kutokana na janga la mlipuko wa virusi vya Corona.

Liverpool - 6

Kwa mara ya kwanza: 1977

Kwa mara ya mwisho: 2019

Ukweli wa kufurahisha: Liverpool ndio klabu iliyofanikiwa zaidi kutoka nchini England kwenye michuano hiyo, ikishinda fainali sita kati ya 10 iliyoweza kufuzu.

Fainali ya Liverpool dhidi ya AC Milan mwaka 2005 bila shaka ilikuwa hitimisho kubwa zaidi katika historia ya mashindano hayo.

Hatimaye wakishinda kwa mikwaju ya penalti, Liverpool walitoka nyuma ya mabao 3-0 kipindi cha mapumziko. Lakini kipindi cha pili waliweza kusawazisha mabao hayo na fainali kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti na Liverpool wakashinda kwa kile kinachoitwa ‘miujiza ya Istanbul’.

Mwaka 2019, Mohamed Salah na Divock Origi walikuwa wameamua mbele ya lango walipoishinda Tottenham kule jijini Madrid nchini Hispania, lakini walipoteza kwa 1-0 kwa Los Blancos katika mchezo mwingine wa fainali msimu uliopita.

Barceloba - 5

Kwa mara ya kwanza: 1992

Kwa mara ya mwisho: 2015

Ukweli wa kufurahisha: Ushindi wa kwanza wa Barcelona mwaka 1992 ulikuwa toleo la mwisho la Kombe la Ulaya kabla ya mashindano hayo kubadilishwa kuwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lionel Messi ameng’ara mara nyingi katika matukio kadhaa ya ajabu na ya kuvutia kwenye mafanikio ya Barcelona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mwaka 2008, mpira wake wa kichwa uliipatia Barcelona ushindi wa kwanza baada ya miaka 16 wakati kikosi cha Pep Guardiola kilipowashinda mabingwa watetezi Manchester United mjini Rome chini Italia.

Miaka mitatu baadaye, Mashetani Wekundu walikuwa tena upande usiofaa dhidi ya Blaugrana, huku Messi akiibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Wembley.

Mnamo mwaka wa 2015, nyota huyo wa Argentina dhidi ya Jerome Boateng na Manuel Neuer aliiweka timu hiyo ya Catalunya kwenye fainali nyingine, ambapo walikwenda kuifunga Juventus mjini Berlin nchini Ujerumani.