Taasisi hizo za serikali zimewasilisha rasimu ya bajeti za taasisi zao leo Machi 19 katika Kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC).Akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Manyara, Mhandisi Dutu Masele, amesema kwa mwaka wa fedha ujao wameweka maoteo ya sh. Bilioni 11.529.Mhandisi Masele alitaja miongoni mwa kazi watakazofanya ni kutanua mlima Dabir na kujenga madaraja mawili katika barabara ya mbuyu wa mjerumani, kuweka taa za barabarani kwenye baadhi ya miji na kujenga mzunguko wa barabara ya Mbulu.Akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Mjini Babati (BAWASA), Mhandisi Honolath Sebastian, amesema wameomba sh. Bilioni 6.247 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji na kuendelea kujenga miradi ya maendeleo.Mhandisi Sebastian amesema miongoni mwa kazi watakazofanya ni kukamilisha mradi wa maji Dareda/Singu na kuendeleza ujenzi wa mradi wa maji wa Magugu.Naye Meneja wa Wakala wa usambazaji maji vijijini (RUWASA) mkoani Manyara, Mhandisi Wolta Kirita, akisoma rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha ujao amesema wameomba sh. Bilioni 20.5 kwa ajili ya miradi 16 ikiwemo uchimbaji wa visima 40.Aidha ameongeza kuwa lengo la bajeti hiyo ni kuongeza upatikanaji wa maji ambapo zaidi ya wakazi 160,000 wanatarajiwa kupata maji.Vile vile Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara za Mjini na vijijini (TARURA), Erick Chenga, amesema wameomba sh. Bilioni 20.716 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.Akiwasilisha Mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 katibu Tawala msaidizi mipango na uratibu Maarufu Mkwaya amesema kwa mwaka ujao wameomba sh. Bilioni 255 ambapo Bilioni 70 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere, amezipongeza taasisi zote za serikali kwa utoaji wa huduma kwa wananchi.
Taasisi za serikali zaomba mabilioni kuboresha huduma
19Mar 2023
Jaliwason Jasson
Manyara
Nipashe Jumapili
Taasisi za serikali zaomba mabilioni kuboresha huduma
MAMLAKA za maji na Wakala za barabara mkoani Manyara zimepitisha bajeti ya sh. Bilioni 58.985 ili kuboresha miundombinu ya maji na barabara kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Wajumbe wa kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Manyara (RCC) wakifuatilia mawasilisho ya rasimu za bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024. Picha na Jaliwasson Jason










