NMB kuwapeleka Dubai washindi nane wa MastaBataKoteKote

29Jan 2023
Na Mwandishi Wetu
MOROGORO
Nipashe Jumapili
NMB kuwapeleka Dubai washindi nane wa MastaBataKoteKote

Benki ya NMB imeendesha droo ya wiki ya mwisho ya Kampeni ya NMB #MastaBataKoteKote katika Manispaa ya Morogoro kwenye tawi la NMB-Wami.

Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Wami, Harold Lambileki (kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki mshindi wa Pikipiki katika droo ya NMB MastaBata kotekote, Aidan Stephen Lukindo (katikati) kutokea Morogoro. Kulia ni Meneja wa Benki la NMB Tawi la Morogoro Business center, Hamis Rashid. Benki ya NMB imeshatoa Pikipiki 10 na 14 mpaka sasa zikiwa ni zawadi kwa wateja wa NMB wanaofanya malipo kupita NMB mastercard au Lipa Mkononi (QR) katika msimu huu wa MastaBata.

Zimesalia siku tatu kuelekea 'Grand finale' ambapo wateja nane watajishindia tiketi ya safari ya kwenda Dubai kwa siku nne Benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.

Kwenye droo za kila wiki, washindi 75 wamejishindia Sh. 100,000 kila mmoja na wa 76 akishinda pikipiki aina ya Boxer. Hii imepelekea jumla yao katika droo zote 10 za kila wiki kuwa 760.

Thamani ya zawadi walizoshinda ni pamoja na Sh. milioni 75 pesa taslimu kwa washindi 750 na Sh. milioni 30 za Boxer 10. Jumla ni Sh.milioni 105 na thamani ya zawadi zote za shindano hili la kuchagiza malipo kidijitali ni zaidi ya Sh. milioni 300.

Kabla ya zoezi la kuwapata washindi wa mwisho 76 wa kila wiki, Meneja wa Tawi la NMB Wami, Harold Lambileki, alisema droo ya kuwapata washindi wa kwenda Dubai itafanyika makao makuu ya benki hiyo wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

Meneja huyo alisema kila mteja wa NMB anayefanya miamala yake kwa kutumia NMB Mastercard na Lipa Mkononi (QR) anayo nafasi ya kushinda zawadi ya safari ya Dubai huku wanaochanja sana na kulipa zaidi kidijitali wakiwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea.

Hata wewe unaweza kuibuka mshindi kwenye droo ya ‘Grand Finale’ wiki ijayo hivyo, usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote