...soda kwenye jua kali vyote vikipalilia uhusiano unawakwamisha mabinti kielimu ili kukabiliana na tatizo hilo, kampeni ya nyingi zinafanywa na mikakati ya kuwanusuru wanafunzi mkoani Dar es Salaam zimeshika kasi.
Mathalani, kuna kampeni ya safari salama bila rushwa ya ngono, inayofanyika kwenye wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Ni katika harakati za kupinga ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wasichana hivyo shule zinapotarajiwa kuanza wiki ijayo madereva wazingatie hilo wawe walinzi badala ya wanaoangamiza wanafunzi.
Katika kampeni hiyo ya safari salama bila rushwa ya ngono inatoa elimu nyumba kwa nyumba, shuleni na vituo vya daladala, bodaboda na bajaj, kuwahamasisha madereva na jamii kuacha kuwarubuni wasichana.Madereva hao wanaodaiwa kuhusika na kuwaingiza wasichana kwenye rushwa ya ngono kwa lifti, wanaelimishwa kuwalinda na kuwasaidia kufika salama shuleni na kurudi nyumbani pia.
Shirika la Wanawake Katika Jitihada za Kimaendeleo (WAJIKI), ndilo linalofanikisha kampeni hiyo kwa kushirikiana na kamati zilizoundwa na madereva hao, wanachama wa shirika hilo.Kwa hiyo elimu ya kupinga vitendo hivyo, isaidie na ulinzi wa watoto ufanikiwe si shuleni, nyumbani na vituoni walipo madereva.
WAJIKI inawahimiza kuacha kulaghai wasichana pia kuwapa na kubandika stika kwenye vyombo hivyo vya usafiri vyenye ujumbe wa safari salama kwa wasichana na wanafunzi bila rushwa ya ngono.
Kwa Dar es Salaam zipo kamati 72 zilizoundwa na madereva wa bodaboda, bajaj na daladala takribani 30,000 wilayani Kinondoni na Ilala.Hivyo mbali na kutoa elimu madereva wawazuie wanafunzi kuzagaa vituoni, lakini wawatafutie usafiri wa haraka, ili wawahi shule au nyumbani wakisafirishwa na daladala hata bajaji na pikipiki kama si eneo lenye umbali mrefu.
Madereva wakumbuke wana jukumu la kuwaokoa wanafunzi na mimba zinazopatikana kwenye lifti.Lakini hata wanafunzi nao waanze kujitambua na kujiamini kuwa kupewa lifti siyo sababu ya kurubuniwa na kujiingiza kwenye uhusiano unaosababisha kuvuruga masomo.
Ni muhimu madereva kujua kuwa kazi yao ni muhimu lakini isiwe chanzo cha kuwaangamiza mamia ya wasichana wa Tanzania kwenye upotovu na kuvuruga maisha yao.
Wazazi, walezi na walimu wanaamini madereva na makondakta wakiamua kuacha kuhadaa wanafunzi ukatili huo wa kijinsia na unyanyasaji havitashamiri katika jamii.
Madereva wasaidie watoto wetu wanapokwenda shuleni kuanzia wiki ijayo wasafiri salama na kutimiza malengo yao ya elimu na kupunguza ukatili wa ngono kwa wanafunzi.
Takwimu za polisi, zinaonyesha matukio ya ukatili kwa watoto yanazidi kuongezeka, kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu yamefikia 6,168."
Kati ya hao wasichana ni 3,287 na wavulana ni 881, huku waliobakwa wakiwa 3,524 na waliolawitiwa ni 637, wavulana ni 567 na wasichana ni 70.Mambo hayaishii hapo waliopata mimba ni 1,887.
Kampeni ya safari salama kwa wasichana na wanafunzi bila rushwa ya ngono inawezekana ianze kuzaa matunda sasa mwaka huu wa 2023 unapoanza na kukomesha ukatili wa kijinsia kwenye jamii na kulinda watoto.Pamoja na madereva kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake kukomesha vitendo hivyo, ikiwamo kutoa za taarifa kwa vyombo vya dola, badala ya kuiachia serikali na asasi za kiraia zinazopambana na ukatili wa kijinsia.
Kwa hiyo mwaka mpya unapoanza madereva, walezi, wazazi timizeni wajibu wa ulinzi kwa watoto ili wasichana wetu na wavulana wawe na hatima bora kielimu.