TADB yaendeleza mageuzi katika sekta ya mifugo

17Jul 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
TADB yaendeleza mageuzi katika sekta ya mifugo

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeshiriki kikamilifu katika Maonesho na Mnada wa mifugo ambao ni mnada wa kwanza kuwahi kufanyika nchini ikiwa na lengo la kuonesha mbegu mbalimbali za mifugo, fursa kwa wafugaji kujifunza ufugaji kibiashara kupata elimu na kubadilishana uzoefu. 

Afisa Mwandamizi wa Maendeleo ya Biashara - TADB, Furaha Sichula (Kushoto) akitoa maelezo kwa wafugaji waliotembelea banda la TADB wakati wa Maonesho na Mnada wa Mwaka ya Mifugo yaliyoratibiwa na Chama cha Wafugaji Mifugo Kibiashara (TCCS).

Maonesho hayo yameratibiwa na Chama cha Wafugaji Mifugo Kibiashara Tanzania (TCCS). 

Akizungumza jana wilayani Chalinze ambapo unafanyika mnada huo, Ofisa Mwandamizi wa TADB, Furaha Sichula alisema hadi sasa TADB imeongeza tija katika sekta ya ufugaji kwa kuwekeza zaidi ya Sh.bilioni 42 ambazo kati ya hizo, bilioni 14.2 zimeenda kwenye sekta ndogo ya nyama ikiwemo ujenzi wa viwanda viwili vya kuchakata nyama.

“TADB pia imetoa bilioni 13.5 imeenda kwenye sekta ndogo ya maziwa ikiwemo viwanda 4 vya kusindika maziwa, Bilioni 7.5 imeenda kwenye sekta ndogo ya kuku na 6.8 imeenda kwenye sekta ya uvuvi wa ufugaji wa Samaki kwenye vizimba,” alisema Sichula

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge (Kulia) akikabidhiwa zawadi alipotembea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakati wa maonesho ya kwanza ya Maonesho ya Mwaka ya Mifugo yaliyoandaliwa na Chama cha Wafugaji Mifugo Kibiashara (TCCS). Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Biashara -TADB Bi. Saunath Tayah. 

Aliongeza kuwa TADB inalenga kufikia Watanzania wengi zaidi katika sekta ya Mifugo, Kilimo na Uvuvi ili kuongeza uchumi wao na maendeleo ya sekta nzima. 

Katika Maonyesho hayo viongozi mbalimbali walitembelea banda la TADB na kuwashukuru kwa jinsi ambavyo wanajitoa zaidi katika maendeleo ya sekta hizo adhimu katika uchumi wa nchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki aliishukuru TADB kwa kuwasaidia katika maeneo mengi na kuomba benki hiyo kutoa msaada zaidi katika kuwezesha mikopo ya sehemu ya malisho ili kuepusha mifugo kuhamahama na kuhama kutoka kufuga kienyeji na kuanza kufuga kibiashara.

Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye (Kulia) akisikiliza maelezo wakati alipotembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ambao ni wadhamini wakuu wa Maonesho ya Kwanza ya Mifugo yaliyoratibiwa na Chama cha Wafugaji Mifugo Kibiashara (TCCS). Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Biashara -TADB, Grayson Ferdinand. 

Mmoja wa mfugaji aliyeshiriki katika maonyesho hayo  Leng’idu Niwuyai alisema TABD imekuwa na mchango mkubwa katika kuwasaidia wafugaji wadogo wadogo kuweza kufuga kisasa kupitia mikopo.

“Tumekuwa tukipata mikopo ambayo imetusaidia sana sisi wafugaji wadogo wadodo kufuga kisasa na hivyo kufanya kazi yetu hii iwe na faida. Tunaiomba TADB iwafikie wafugaji wengi Zaidi ili kuongeza tija kwa sekta hii husasani kwa wafugaji wado wadogo,” alisema

Afisa Tehama Mwandamizi - TADB, Mwenze Kabinda (Kulia) akitoa maelezo kwa mfugaji aliyetembelea banda la TADB wakati wa Maonesho na Mnada wa Mwaka ya Mifugo yaliyoratibiwa na Chama cha Wafugaji Mifugo Kibiashara (TCCS). TADB ni mdhamini Mkuu wa Maonesho haya ambayo ni ya Kwanza kuwahi kufanyika ikiwakutanisha wafugaji mbalimbali.