Kijana William (19) ajinyonga Gest

17Jul 2022
Na Mwandishi Wetu
Geita
Nipashe Jumapili
Kijana William (19) ajinyonga Gest

WILLIAM Bahelo (19) mkazi wa Wilaya ya Geita amekutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga akiwa ndani ya nyumba ya kulala wageni (Gest House) inayomilikiwa na Baba yake mkubwa iliyopo katika Mtaa wa Mbugani mkoani Geita, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugomvi wa mali za familia.

Akizungumza na chombo kimoja cha Habari, Shangazi wa marehemu huyo Kabula Nairobi, amesema hajui chanzo cha tukio hilo huku akiliomba Jeshi la Polisi kuchunguza kifo cha mtoto wake.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita Henry Mwaibambe, kwa njia ya simu amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku akisema Jeshi linaendelea kuchunguza kifo cha kijana huyo ambacho kinahusishwa na ugomvi wa mali za Familia.

Aidha Kamanda Mwaibambe amezitaka Familia kuendelea kushirikiana katika kupunguza matukio haya ambayo yamekuwa yakiendelea juu ya ugomvi wa mali za Familia.