Tangu mwaka jana ulipoanza mchakato wa sensa hiyo, yamesemwa mengi na baadhi ya Watanzania ambayo ninadhani ipo haja ya kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ili watu wawe na uelewa wa kutosha kuhusu sensa.
Kwa nini? Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwamba kwenye sensa kuna dodoso linalohusiana yasiyohusiana, jambo ambalo wakati mwingine linaweza kuleta mkanganyiiko.
Ninakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan, alishalitolea ufafanuzi kuwa hayo potofu hayapo, lakini huko mitaani na vijiweni, wapo baadhi ya watu wamekuwa wakilizungumzia wakidai kuwa lipo dodoso la aina.
Wakati kukiwa na madai kama hayo, wengine wamekuwa wakihusisha sensa hiyo na chanjo ya UVIKO-19, kwamba inalenga kujua idadi ya Watanzania waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.
Kuna wakati Kamisaa wa Sensa, Anne Makinda alilikemea hilo na kuwataka watu waache na imani potofu na kufafanua kwamba sensa haihusiani na chanjo hiyo ingawa ni muhimu kupata chanjo.
Hivyo kwa hali kama hiyo, ni vyema wakati huu wa kuelekea kwenye sensa, kasi ya utoaji wa elimu ikaongezeka ili kuhakikisha watu wanaachana na upotoshaji huo ambao unaweza kusababisha baadhi ya watu wasihesabiwe.
Kama watoaji elimu watakuwa ni wachache, basi si vibaya idadi ikaongezwa ili kuharakisha kazi hiyo kwa umma wa Watanzania kwa lengo la kuepusha upotoshaji unaoendelea mitaani.
Ninaamini kwamba kwa jinsi ambavyo maandalizi ya sensa yanavyoendelea, ikiwamo kutumia utaratibu wa anwani za makazi, mpango shirikishi ulioandaliwa kati ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar wa kutekeleza kazi hiyo unaweza kusaidia, iwapo.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba, unaweza kusaidia kufanya vizuri katika sensa hiyo, iwapo Watanzania wataelimishwa vya kutosha nakuacha na elimu nyingine ambazo wamekuwa wakipandikiziwa.
Kwa kuwa utaonyesha ni wapi kila mwanachi anapoishi, utasaidia pia serikali kupanga mipango ya maendeleo, kuimarisha usalama, kuongeza ajira na mapato ya serikali.
Serikali hutumia sensa ili kujua jinsi ya kupanga na kukadiria matumizi ya raslimali na fedha, pia wanasiasa hutumia idadi ya watu na maeneo walioko kutathmini azma zao za kisiasa.
Hayo mengine yanayoenezwa mitaani kwamba inalenga kujua idadi ya Watanzania waliochanja au suala la dini, yasingepewa nafasi kama jamii itapewa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa sensa.
Kuwapo mkanganyiko huo ndani ya jamii, ni wazi kwamba bado wapo baadhi ya Watanzania ambao hawajajua umuhimu wa sensa, ingawa imekuwapo tangu mwaka 1963.
Ikumbukwe kuwa serikali inaweza kushindwa kupanga shughuli zake za maendeleo iwapo haitakuwa na takwimu sahihi za idadi ya Watanzania, hivyo ninadhani ni muhimu kila Mtanzania kuhesabiwa.
Hiyo inaweza kufanikiwa iwapo wote tutakuwa na kauli moja kwamba tuwe tayari kuhesabiwa Agosti 23 badala ya kuwapo wengine wanaopenyeza elimu nyingine yenye lengo la kukwamisha sensa.
Watu wenye mawazo hayo ni vyema wakakumbushwa kuwa bila idadi ya Watanzania kujulikana, ni vigumu kwa serikali kufanikisha malengo ambayo imejiwekea ya kuwahudumiwa wananchi wake.
Pamoja na hayo, ni muhimu kutambua kuwa si kuhesabiwa tu, bali pia wajibu wa kila Mtanzania kutoa maelezo sahihi yanayomhusu, ambayo kimsingi ndiyo serikali inachohitaji.
Iwapo kutakuwa na mtu ambaye amejipanga kutoa taarifa za uongo kwa sababu ya kuhofia suala la udini au chanjo, ni wazi lengo la sensa halitatimia na pia atakuwa ameikwamisha serikali yake.
Nimalizie kwa kurudia kuwa, ni wakati sasa wa kuendelea kutoa elimu zaidi kwa umma, ili utambue na kuepuka ushawishi mwingine wa mitaani wenye lengo la kukwamisha sensa sensa hiyo.



.jpg?itok=nfwjwDzv)







