Winnie anayemilikia lebo la W Style Loft alitangazwa kushinda shindano hilo kutokana na uwezo wake wa kutumia ubunifu kubuni mavazi kwa umaridadi hasa akitumia nakshi za kanga katika kukoreza ubora wa kazi zake.
Akizungumzia kuhusiana na ushindi huo, Winnie alibainisha kuwa kwa muda ambao amekuwa akishiriki kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi amekuwa akithamini zaidi katika ubora wa kazi na ubunifu wa umakini.
Alisema kuwa amekuwa akitumia muda wake mwingi kujifunza ubunifu wa mavazi kwa njia mbalimbali hasa kwa kuwaiga wabunifu wakubwa na wenye mafanikio katika ubunifu wa mavazi.
Amewasihi wabunifu wa mavazi kuongeza thamani katika utendaji wao wa kazi ili kuendana na kasi ya serikali ya sasa inayotaka kuona sanaa inakuwa na hususan sanaa ya ubunifu wa mavazi.
Kwa upande wake Mratibu wa Onesho la mwaka huu la Lady in Red lililoandaliwa na kampuni ya uandaaji wa matukio na upambaji wa dhifa, Hugo Domingo, Mary Fernandez alibainisha kuwa kwa mwaka huu onesho limekuwa na faida kubwa kwa kuwa limetoa wasaha kwa wenye ulemavu kuonesha kazi zao za kibinifu na kuahidi kuendelea kuwasidia.










