Wafanyabiashara 200,000 kuanza kugaiwa bure EFDS

21Jan 2016
Nipashe
Wafanyabiashara 200,000 kuanza kugaiwa bure EFDS

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea na maandalizi ya manunuzi ya mashine za kielektroniki za kodi (EFDs) kwa ajili ya kuanza kuzigawa bure kwa wafanyabiashara stahiki.

rais dk.john magufuli akisalimia na wafanyabiashara

Wafanyabiashara wanaolengwa kupatiwa mashine hizo katika awamu ya kwanza ni 200,000 wenye maduka ya vipuri, mawakili, maduka ya jumla, wafanyabiashara wakubwa wa mbao, migahawa mikubwa, maduka ya simu na vipuri vyake, baa na vinywaji baridi, studio za picha, huduma za chakula, wauzaji wa pikipiki, maduka makubwa ya nguo na biashara nyingine.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipakodi TRA, Richard Kayombo, alisema mamlaka hiyo ipo kwenye maandalizi ya ununuzi wa mashine hizo na zikishanunuliwa zitaanza kugawiwa kwa wafanyabiashara hao.
Alisema uchambuzi wa wafanyabiashara wanaostahili kupewa mashine hizo unaendelea nchi nzima kwa kuangalia ukubwa wa biashara ili kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi.