Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas wakifuatilia kwa umakini tamasha la Xtra Uni Bash lililoandaliwa na kituo kimoja cha redia na kudhaminiwa na Bia ya Guinness Smooth inayotengenezwa na kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na makampuni mengine. Tamasha hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ekwabi Mujungu (kulia) alizungumza na wasanii( hawapo ) pichani wakati wa ufunguzi wa kongamano la kuelimisha vikundi vya sanaa. Kushoto ni kaimu msaidizi ofisi ya Rais sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele.
Mwandaaji wa filamu nchini, Aziz Mohamed akiwa na baadhi ya wasanii na wadau wa sanaa wakati wa uzinduzi wa kipindi kipya cha mahusiano cha ‘Date my Family’ ambacho kitaanza kuonyeshwa kuanzia leo kwenye king'amuzi cha chaneli ya Miasha Magic Bongo ya DSTV. PICHA: MPIGAPICHA WETU
Deogtratius Killer (mwenye shati nyeupe), akicheza na wanenguaji wake kwenye onyesho la bendi hiyo mwishoni mwa wiki mjini Morogoro. PICHA: SABATO KASIKA
Msanii wa bongofleva nchini Rashid Abdallah maarufu kama Chid benz akimweleza jambo Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza.