“Naitwa Omary William waSombetini, Arusha. Nawashauri wadau wa Yanga tuanze sasa maandalizi ya kufanya klabu yetu pendwa ijitegemee kiuchumi. Kwa kuanzia tuanze na mtajiwa wanachama.
"Bidhaaza Yanga na mechi za kirafiki kwenye viwanja vya mikoani hususan kipindi cha maandalizi ya msimu mpya. Je, viongozi na wadau wafanye nini?
“Tuachanena ada ya 1,000/- kwa mwezi. Maisha yamepanda basi angalau tulipe 10,000/- kwa mwezi na hilo lipo ndani ya uwezo wawanachama walio wengi.
“Viongoziwaandaeoperesheni ‘saidia Yanga ijenge uwanja ndani ya mwaka mmoja.’Tutamiliki uwanja wetu nasi lazima iwe katikati ya Jiji. Hata nyumba huwa tunaanza kujenga vijiji ninabaadayemijini.
“Kama wapenzi wa Yanga tunatoka mikoani kwenda Dar es Salaam kuishuhudia Yanga inapocheza, vipi tushindwe kugharimia usafiri wa buku (elfu) mbili?
Naamini tukiamua tutafanikiwa kwani ‘Yanga Daima Mbele Nyuma mwiko.’Asanteni kwa kumrudisha mnyama msituni. Msimbazi kimyaa …
“Wanachama waelimishwe kuhusu umuhimu wa wao kuichangia timu yao. Kwa mfano kuingia uwanjani kwa wingi na kulipa viingilio halali. Kuchangiakwaharambeenakununuabidhaahalaliza Yanga.
“Naamini tukipitisha harambee ya 10,000/- na kuendelea tutapata uwanja wa mazoezi na mechi ndogondogo. Kama mtu wa kawaida anaanzisha shule na kujenga uwanja mzuri wa michezo kwa nini wana-Yanga tushindwe?
“Tukiwa na nia ya dhati kabisa ni lazima tutafanikiwa. Tulipe ada na kuongeza wanachama wapya.”
Mwenye namba 0784 580022 alinitumia ujumbe huu:
“Asante kwa kuandika ukweli kuhusu uchumi na utegemezi. Sisi wapenzi wa Yanga tunaguswa mno na timu yetu kukosa vyanzo vya mapato. Tutajitegemealini?
“Sisi wapenzi tutaiimarishaje timu? Hatakupitia kwenye mitandao ya simu tufanye hivyo ili kuiimarisha Yanga yetu.”
Mpenzi mwingine aliandika: “Umeongea ukweli mtupu mzee wangu. Wana-Yanga wengi tunaojitambua tuna umizwa sana na hali hii ingawa najua wengine tunaotafakari kwa matumbo tutakubeza. Usichoke kuongea ukweli – 0716 171919.”
Kwa umriwa klabu ya Yanga iliyoanzishwa mwaka 1935, halafu uambiwe haina mbele wala nyuma (ingawa kauli mbiu yake ni ‘Daima Mbele Nyuma Mwiko) inasikitisha na kushangaza.
Hivi kweli viongozi wote (waliopita) walishindwa na waliopo wameshindwa kuwahamasisha mashabiki na wanachama kuhusu umuhimu wa klabu kujigemea?
Au malengo yao ni kujinufaisha kupitia mgongo wa Yanga? Kinachonishangaza zaidi, hata mashabiki na wanachama twaridhika na utegemezi huu!
Hali hii yanikumbusha walivyosema wahenga kuwa “aliyezoea kupokea, kutoa ni vita.” Maana yake mtu aliyezoea kupokea vitu huwa hawezi kutoa kwa urahisi.Methali hii huweza kutumiwa kumpigia mfano mtu bahili au mgumu wa kutoa vitu vyake ingawa anapenda vitu vya kupewa.
Ndivyo tulivyo wana-Yanga! Tuzinduke ili tuondokane na utegemezi huu kwani twajifedhehesha.
marobarnabas@yahoo.com
0715/0784 33 40 96


.jpg?itok=nfwjwDzv)








