Mwamuzi Mark Clattenburg alimwonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Mertesacker katika dakika ya 18 kwa kosa la kumwangusha Costa ndani eneo la hatari.
Mshambuliaji aliyehusika pia na tukio lililosababisha Gabriel kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi baina ya timu hizo mwanzoni mwa msimu huu, ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo dakika tano baadaye na kumwacha Wenger akiwa amechanganyikiwa.
"Tulikuwa na kazi ngumu ya kupanda mlima tukiwa watu 10, lakini naamini pamoja na hali hiyo, tulistahili sare ya 1-1," alisema Wenger wakati akizungumza na Sky Sports.
"Hatutaki kuzungumzia uamuzi wa refa. Costa amesababisha wachezaji wetu wawili kutolewa nje kwa kadi nyekundu, hivyo ana akili sana."
Aliongeza: "Katika mchezo wa kwanza, tulimkosa Gabriel (kadi nyekutu), safari hii Mertesacker naye ameonyeshwa kadi nyekundu.
Kwamba Costa aliguswa au hakukuswa, hiyo itabidi niangalie tena marudio ya mechi ili nijiridhishe. Simlaumu kwa lolote, lakini hiyo imetokea na ndivyo soka ilivyo."
Kipigo hicho ina maana Arsenal haijawahi kutoka na ushindi katika mechi tisa za mwisho ilizocheza na Chelsea Ligi Kuu England.
"Ni aibu kubwa kwetu kuwekeza nguvu nyingi kwenye mchezo ambao baada ya dakika tisini hakuna tulichoambulia," alisema.
"Kwa jumla, tulifanya kila lililowezekana hadi dakika ya mwisho na nadhani tulistahili angalau sare ya bao 1-1 pamoja na kucheza muda mrefu tukiwa wachezaji 10 uwanjani."
Wenger: Diego Costa ana akili sana
26Jan 2016
Nipashe
Wenger: Diego Costa ana akili sana
LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger amemtaja mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kama mchezaji mwenye 'akili' baada ya kuhusika katika tukio lililosababisha beki Per Mertesacker kupewa kadi nyekundu isiyo na onyo katika mchezo waliolala bao 1-0 dhidi ya The Blues kwenye Uwanja wa Emirates.










