Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, meneja wa timu hiyo, Mohamed Hussein alisema lengo la kuweka kambi Morogoro ni kutaka kubadilisha hali ya hewa ambayo mkoani humo inatofautiana kidogo na Dar es Salaam.
"Tumesikia huko kuna joto kali, tumeamua kuweka kambi Morogoro ili tuweze kumudu hali ya hewa ya Dar es Salaam tutakapokuja kupambana na hao wanaojiita 'Wakimataifa'," alisema Hussein.
Alisema kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda mechi hiyo pamoja na kutambua kuwa wanacheza dhidi ya timu ngmu.
Aliongeza kuwa kikosi chake hakina majeruhi na wamejipanga kupambana kuhakikisha wanapata pointi kwenye mchezo huo wa ligi ya Bara.
Mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 50 wamecheza mechi 21 wakati Kagera Sugar yenyewe imeteremka uwanjani mara 24 na imejikusanyia pointi 25.










