Beki Kessy mbioni kulamba 'dume' Msimbazi

28Feb 2016
Mahmoud Zubeiry
Dar
Nipashe Jumapili
Beki Kessy mbioni kulamba 'dume' Msimbazi

KWA wiki nzima beki-chipukizi wa pembeni Msimbazi, Hassan Kessy amekuwa kiini cha habari baada ya pasi yake ya kizembe kwenda kwa kipa wake kwenye mchezo dhidi ya Yanga, kuipa bao la kuongoza timu hiyo ya Jangwani iliyokwenda kushinda 2-0 baada ya dakika tisini.

beki-chipukizi wa pembeni Msimbazi, Hassan Kessy .

Pamoja na baadhi ya mashabiki wa Simba kutaka mchezaji huyo kutemwa kwa kosa hilo, klabua yake imefunga masikio na sasa imeamua kuanza mchakato wa kumwongezea mkataba.

Rais wa Simba, Evans Aveva alisema mwishoni wa wiki hii kuwa, mkataba wa beki huyo unakwenda ukingoni, lakini kutokana mahitaji myaliyopo kwa sasa kwenye safu ya ulinzi, wameamua kuzungumza naye ili aendelee kuvaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe.

Aveva alisema mazungumzo ya mkataba mpya wa Kessy yalikwamishwa na Meneja wa mchezaji huyo, Athumani Tippo.

Tumelazimisha yafanyike, ili matokeo yoyote ya mchezoni yasije yakaathiri hili baadaye,"alisema Aveva. Hata hivyo, Aveva alikiri kuwa kosa lililofanywa na beki huyo kwenye mchezo dhidi ya Yanga limemharibia kwa kiasi fulani.

Nisingependa kuzungumzia suala hili, makosa kwenye soka ni mambo ya kawaida," alisema bosi huyo.