Mkaguzi wa mbegu kutoka (TOSCI), Nugwa Fortunatus amesema hayo katika mafunzo waliyofanya kwa waandishi wa Habari mkoani Morogoro yaliyofanyika mkoani hamo.
Fortunatus anasema wapo wakulima wanatumia mazao waliyovuna mashambani mwaka uliopita kama mbegu na baadae kuja kulalamikia makampuni ya mbegu wakipata mazao kidogo tofauti na matarajio yao.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Thadei Hafigwa anasema mafunzo kama hayo kwa waandishi wa Habari ni mazuri ambayo yatamjenga mwanahabari katika kuelimisha wakulima sambamba na kuwa mkulima bora.
Amesema wakulima wanapaswa kutambua kuwa kwa kutumia miongozo, taratibu na sheria za mbegu zilizopo wanaweza kulima na kupata mazao yenye tija.
Akizungumza kwenye kikao hicho Afisa kutoka taasisi inayoshughulika na mifumo ya masoko ya kilimo (AMDT), Joseph Mosha amesema mkulima anapaswa kuhakikisha amenunua mbegu bora zilizothibitishwa na TOSCI zitakazomsaidia kupata mazao bora na kupata mavuno bora bila kupata hasara.