Safari Lager Cup kutimua vumbi kesho, kusaka vipaji

12Jan 2024
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Safari Lager Cup kutimua vumbi kesho, kusaka vipaji

Michuano ya Safari Lager Cup inaendelea na hivi sasa ipo katika ngwe ya pili kutafuta wachezaji 16 kati ya 22 waliochanguliwa kucheza katika mikoa 4: Mbeya; Mwanza; Arusha na Dar es Salaam.

Katika kuendeleza vipaji vya vijana kusaka mabingwa wapya katika soka ndani ya Safari Cup, vijana 22 wenye vipaji, watachaguliwa kutoka mikoa hiyo ili kujenga 'cream dream team' ya Safari Champions itakayocheza na timu kubwa ya kimataifa hapo baadae.

⁠Makocha pamoja na Watumiaji wa bia ya Safari Lager na wapenzi wa soka kiujumla, watapigia kura vijana hawa ili kuchagua viijana hao 22 mabingwa wapya wa Soka.

Tarehe 13 Januari muendelezo wa michuano itafanyika ndani ya Mwanza katika viwanja vya Nyamagana kuanzia saa 8 mchana na Mbeya katika viwanja vya Soweto - Mwenge pamoja kuanzia saa 10 jioni.

- Ili kufatilia kwa karibu taarifa za michuano ya Safari Lager Cup tembelea mitandao ya kijamii - Instagram @safarilager_tanzania | Facebook: @safarilager | Twitter/X: @safarilagertz pamoja au tovuti www.safarilager.co.tz- #SafariLagerCup #MabingwaWapyaWaSoka #SafariLager