Klopp afungiwa mechi mbili EPL

20May 2023
Na Waandishi Wetu
UINGEREZA
Nipashe
Klopp afungiwa mechi mbili EPL

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amefungiwa mechi mbili kwa kumkashifu mwamuzi, Paul Tierney.

 

Klopp amesimamishwa na kutozwa faini ya pauni 75,000 kufuatia maoni yake kwa vyombo vya habari baada ya mechi dhidi ya Tottenham Hotspur iliyochezwa Aprili 30, mwaka huu,  Chama cha Soka cha England (FA), kilisema jana.

Baada ya ushindi wa Liverpool wa mabao 4-3 nyumbani, Klopp alimshutumu mwamuzi, Tierney kwa kuwa na kitu "dhidi" ya Liverpool.

FA ilisema mechi ya kwanza ya marufuku ya Klopp ya kufungiwa kwa laini ya kugusa ilianza mara moja na ya pili ilisimamishwa hadi mwisho wa msimu wa 2023-24, kwa sharti hatakiuka tena Sheria ya FA ya E3 kwa sasa.

Uamuzi huo unamaanisha Mjerumani huyo hatoisimamia timu yake leo watakapoikaribisha Aston Villa.

Liverpool iko katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 65, pointi saba mbele ya Brighton & Hove Albion walio nafasi ya sita lakini wamecheza mechi mbili zaidi.