Hata hivyo, imeshindwa kuweka rekodi ya kushinda mabao 6-0 kama ilivyofanya kwenye mechi mbili zilizopita.
Yanga ilianza ligi hiyo inayopigwa kwenye Uwanja wa Kituo cha Ufundi TFF Kigamboni kwa kuivurumusha African Sports mabao 6-0, kabla ya kushinda kwa idadi hiyo ya mabao kwa mara ya pili dhidi ya Green Warriors.
Ni matokeo yanayofanya kuendelea kusimama juu ya msimamo wa ligi ikiwa na pointi tisa, ikishinda mechi zote tatu.
Mabao ya washindi yaliwekwa wavuni na Mahmoud Bugoma, Nasri Halifa na Ahmed Mohamed.
Wakati vijana wa Yanga wakifanya vitu vyao, kikosi cha Simba chini ya miaka hiyo nacho kikaiadhibu KMC mabao 2-0, moja likiwa ni la kujifungwa mwenyewe, Steven Kimaro, na lingine likiwekwa kwenye kamba na Hamis Salum.
Kwa matokeo hayo, Simba inafikisha jumla ya pointi saba kwani mechi iliyopita iliifunga JKT Tanzania bao 1-0, lakini mchezo wa ufunguzi ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ihefu.
Matokeo mengine ya ligi hiyo, Ruvu Shooting ilitoka sare ya bao 2-2 dhidi ya Singida Big Stars, African Lyon ikaitwanga JKU Academy 3-1, Azam ikaibugiza Pan African 4-0, Mbeya Kwanza na Karume Youth Centre zikatoka sare ya bao 1-1, Ihefu ikaiadhibu JKT Tanzania 2-0 na African Sports ikashinda 1-0 dhidi ya Green Warriors.










