Ambapo wanatarajia kucheza kesho jioni dhidi ya APR ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amahoro.
Yanga ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao, Clement Sanga ilitua na kwenda moja kwa moja kwenye hotel ya ‘The Mirror’ na kisha wakafanya mazoezi jioni ya jana kwenye Uwanja wa mazoezi wa Shirikisho la Soka Rwanda (Ferwafa).
Yanga ilikuwa na watu 35 ambao waliwasili kwaajili ya mchezo huo ambapo kati ya idadi hiyo, nane ni viongozi wa juu wa klabu, saba ni wataalamu wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji 20.
Pluijm adai ushindi wao
Kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van Der Pluijm alisema ninafuraha kufika nchini Rwanda na ninafurahi kuona pale anapotoka kiungo Haruna Niyonzima lakini dhamira yetu kubwa ni kupata ushindi.
“Ninaifahamu APR, na ninataka kuishinda. Naamini kila kitu kinawezekana kwenye mpira hivyo sina shaka naamini tutaishinda kwani nimeshafahamu staili yao ya uchezaji lakini pia viwango vya wachezaji wao.
“Wanaonekana kuwa na wachezaji walioimarika kiafya na wenye uwezo mzuri. Mimi pia nina wachezaji wazuri na nina jiamini kuwa wataweza kunipa matokeo mazuri kama yale ambayo tumekuwa tukiypata kwenye Ligi kwa siku za hivi karibuni.
“Sina presha wala wachezaji wangu hawana wasiwasi na hii inanipa nguvu kuwa nitaweza kushinda kwa kishindo dhidi ya APR kwasababu nimeshawaelewa wanavyocheza na ni matarajio yangu kuwa wachezaji watafanya vizuri,”alisema huku akidai kuwa angependa kuona wachezaji wakicheza kama walivyocheza kwenye ushindi wao wa Ligi Kuu Bara wa bao 5-0 dhidi ya African Sports.
Nahodha Bossou
Nahodha wa Yanga, Mtogo Vicent Bossou alisema kuwa yeye pamoja na wenzake wanandoto za kufika mbali kwenye michuano hii hivyo wamejipangia mikakati ya kushinda kila mchezo unaokuja mbele yao ili kuweka rekodi ya kipekee.
“Tuna kazi kubwa ya kuifanyia Yanga, tutatumia juhudi zetu kushinda dhidi ya APR ili tuweze kujijengea mazingira mazuri ya kucheza hatua inayofuata ya michuano hii ya Klabu Bingwa Afrika,”alisema.
Muro: Lazima Yanga ishinde
Msemaji wa Yanga, Jerry Muro alisema kuwa wamejipanga kufanya vizuri na kwamba APR ni timu nzuri lakini Yanga ni timu nzuri zaidi.
“Tumejipanga kushinda na lazima tushinda, Yanga ni timu kubwa na timu kongwe hivyo hakuna cha sare, ni lazima Yanga ichomoke na ushindi,” alisema.
Tambwe, Ngoma gumzo
Yanga ilimekusanyia mashabiki wengi kila kona ya jiji la Kigali na gumzo kubwa ni uwezo wa washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe. Wachezaji hao wameonekana kuwa tishio na pengine watavuta mashabiki wengi kwenye mcezo wa kesho.
Yanga haikusafiri na wachezaji; Malimi Busungu, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Benedict Tinoco ambao wote ni majeruhi










