Mashindano hayo ya Dubai yamepangwa kufanyika Aprili 23 na Tanzania imepewa nafasi hiyo kutokana na ombi la Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kupeleka wanariadha wake.
Kocha mkuu wa timu ya taifa, Francis John, alisema wanariadha hao wanaendelea na mazoezi kwenye kambi ya timu hiyo mkoani Kilimanjaro.
Mbali na wanariadha hao watatu, Fabian Joseph anatarajia kwenda Japan kushiriki katika mashindano mengine ya kusaka viwango vya Olimpiki yatakayofanyika Aprili 17.
Kocha huyo alisema RT bado inaendelea kutafuta mashindano mengine ambayo yanatambuliwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) ili wanariadha wote wanaounda timu hiyo wapate fursa hiyo muhimu.
Mpaka sasa ni wanariadha wawili tu wa Tanzania ndiyo waliokata tiketi ya kwenda Brazil kushiriki michezo ya Olimpiki. Wakata upepo hao ni Said Makula na Alphonce Felix.










