Katika mechi hiyo iliyokuwa kali na yakusisimua huku ikihudhuriwa na umati wa watu wilayani humo, Wanamaji FC walipata ushindi huo katika dakika ya 29 kupitia kwa Nicolas Antony baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Riziki Abega.
Bao hilo lilidumu hadi dakika ya mwisho licha ya jitihada Za Shirati Mji FC kwani ngome ya ulinzi ya Wanamaji ilikuwa imara kwa dakika zote 90.
Mgeni rasmi katika mchezo huo wa fainali alikuwa Ofisa Michezo wa Mkoa wa Mara, Makondo Makondo, huku pia ukihudhuriwa na mdhamini wa Umoja Cup Rorya, Peter Owino.
Akikabidhi zawadi kwa washindi Ofisa Michezo wa Mkoa wa Mara, Makondo alisisitiza umuhimu wa wadau wa michezo kujitokeza wilayani hapo na mkoa wa Mara kwa ujumla ili kusaidiaana na Owino kuinua vipaji vya soka.“Tumsaidie Peter Owino ili mashindano haya yanayokuwa kila mwaka yazidi kuimarika,” alisema.
Kwa kutwaa ubingwa huo Wanamaji waliibuka na kombe pamoja na Sh. 500,000, wakati Shirati Mji FC ikiondoka na Sh. 150,000 na seti moja ya jezi kwa kumaliza nafasi ya pili huku tuzo ya heshima ikienda kwa, Christopher Owinjo Nyatega.