Msemaji wa Chama cha Karate Tanzania, Salma Abdallah, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi wachezaji wa hapa nchini ili waufahamu vyema mchezo huo.
"Mafunzo hayo yatawasaidia wachezaji kuufahamu vizuri mchezo huu pamoja na kujiandaa kufanya vyema kwenye mashindano yaliyopo mbele yetu," alisema Salma.
Aliongeza mchezo huo kwa sasa unazidi kupata umaarufu tofauti na miaka ya nyuma jambo ambalo linasaidia kuutangaza.
"Tunafurahi kuona sasa mchezo unapendwa, vipaji vipya vinazaliwa, tunaomba Watanzania wajiunge na mchezo wetu," aliongeza.










