Akizungumza na Nipashe juzi, Kocha wa Toto, John Tegete alisema kipigo hicho kimeasikitisha, lakini hawataka kata tamaa kupambana kupata ushindi kwenye mechi zingine.
Alisema anafahamu ugumu wa mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na ukweli kuwa timu zote zimejiandaa vizuri.
“Kwa sasa tunajiandaa dhidi ya Mbeya City, tunajua ni timu nzuri lakini tumejipanga kukabiliana nayo na kupata pointi tatu," alisema Tegete.
Alisema michezo michache waliyonayo mkononi kabla ya ligi kumalizika watahakikisha wanashinda ili kumaliza ligi katika msimamo mzuri.
"Kumaliza ligi wenye nafasi nzuri ni rekodi kwetu, lazima tuhakikishe tunashinda mechi zilizobaki ili pia kurejesha furaha kwa mashabiki," alisema.










