Simba yakomaa mbio za ubingwa

03May 2016
Na Waandishi Wetu
Nipashe
Simba yakomaa mbio za ubingwa

MATOKEO ya sare ya bila kufungana dhidi ya Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara mwishoni mwa wiki iliyopita, haijaikatisha tamaa Simba inayodai bado iko kwenye mbio za kutwaa taji.

kikosi cha simba

Kimahesabu, sare ya timu hizo imefunga njia ya Yanga kutetea taji lake iwapo itafanya vizuri kwenye mechi zake zilizobaki zote wakicheza ugenini.

Kocha Msadizi Simba, Abdallah Hussein amesema kikosi chake bado kimo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na kutoka sare ya bila kufungana na Azam FC mwishoni mwa wiki iliyopita.

Simba iko nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 58, ikitanguliwa na Azam FC pointi 59 na Yanga wanaoongoza kwa pointi 65.

Akizungumza mara baada ya mchezo, Hussein alisema matokeo hayo hayajawakatisha tamaa kwani bado wana nafasi ya kushinda mechi zilizobaki na wapinzani wao kupoteza.

"Hatujakata tamaa, bado tuna uwezo wa kuwa mabingwa msimu huu. Kuna mechi zimebaki kabla ya ligi kumalizika," alisema Hussein.

Simba inajiandaa na mazoezi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mwadui FC wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Wakati huohuo, sare ya bila kufungana dhidi ya Azam FC ni ya kwanza kwa Simba msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa, wanautumia kama uwanja wa nyumbani.

Kabla ya hapo, rekodi zinaonyesha kuwa Simba haikuwahi kutoa sare Taifa.Kadhalika, sare hiyo ni ya pili kwa Azam kwenye Uwanja wa Taifa, ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.

Hata hivyo, kikanuni, mechi ya mzunguko wa kwanza Simba ilihesabisha kuwa inacheza ugenini, huku Azam ikiwa nyumbani.