Wakati Wanajangwani wakifunga mabao 16 na kufungwa sita katika mechi zote nane walizocheza Januari, wapinzani wao wa jadi walikusanya pointi 12 ndani ya mwezi huo na kujisogeza kwa hatua moja hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL wakiing'ia Mtibwa Sugar.
Katika mechi zote tisa za mwezi uliopita (nne za Kombe la Mapinduzi na moja ya FA), kikosi cha Mayanja hakikupata kadi nyekundu, huku wakipewa penalti moja iliyofungwa na Mganda Hamis Kiiza katika ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Kikosi cha Mdachi Hans van der Pluijm, kilipewa penalti mbili (kilikosa moja) na kupata kadi nyekundu moja (Kelvin Yondani dhidi ya Coastal Union) katika mechi zote nane za mwezi uliopita (nne za Kombe la Mapinduzi na moja ya FA), huku timu mbili kilizocheza nazo (Azam na Mtibwa) zilipata kadi nyekundu (John Bocco upande wa Azam na Henry Joseph wa Mtibwa).
Mabao 16 ya Yanga mwaka huu yamefungwa na wachezaji 10. Nyota hao na mabao yao kwenye mabano ni Tambwe (4), Donald Ngoma (3) na Simon Msuva (2).
Wengine ambao kila mmoja amefunga bao moja ni Paul Nonga, Malimi Busungu, Issoufou Boubakar, Yondani, Thaban Kamusoko na Matheo Anthony.
Wachezaji nane ndiyo waliofanikiwa kufunga mabao 15 ya Simba mwaka huu. Wakali hao wa kufumania nyavu na idadi ya magoli yao kwenye mabano ni Kiiza (6), Awadh Juma (2), Ibrahim Ajibu (2), Jonas Mkude (1), Danny Lyanga (1), Said Ndemla (1), Hassan Kesy (1) na Hajji Ugando (1).
Simba yaizidi Yanga Januari
02Feb 2016
Sanula Athanas
Nipashe
Simba yaizidi Yanga Januari
- Timu hiyo ya Msimbazi ilishinda mechi zote nne za Ligi Kuu ikifunga mabao 15 katika mechi 9 za mashindano yote pasi na kadi nyekundu hata moja.
SIMBA na Yanga ndizo timu kongwe zaidi zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu.
Ikiwa chini ya Muingereza Dylan Kerr, Simba ilikuwa na mwenendo wa kusuasua, lakini ujio wa kocha mkuu wa muda, Jackson Mayanja umeonekana kuwa na tija Msimbazi baada ya timu hiyo kushinda mechi zote nne za VPL mwezi uliopita (tatu chini ya Mganda huyo).









