Sh. milioni 490 zavunwa Taifa

22Feb 2016
Somoe Ng'itu
Dar
Nipashe
Sh. milioni 490 zavunwa Taifa

MECHI ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu Bara Yanga na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, imevuna Sh. milioni 490.

Mashibiki wa Simba na Yanga

Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa wenyeji wa mchezo huo, Yanga wametia mfukoni Sh. milioni 139, wakati wageni Simba wamelamba Sh. milioni 99.

"Mechi imeingiza Sh. milioni 490. Tiketi za Sh. 7,000 na VIP A Sh. 30,000 ziliuzwa sote zilinunuliwa," alisema kiongozi mmoja wa Simba, ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti kwa kuwa siyo msemaji.

Katika mchezo huo, Yanga ambao ni mabingwa watetezi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kufikisha pointi 46 zilizowafanya pia warejee kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.

Mabao katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa mwanamke, Jonesia Rukyaa yalifungwa na Donald Ngoma na Amissi Tambwe.