Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo 21 kwa Kanda mbalimbali ikiwemo wasanii bora, waandishi wa habari,wajasiliamali na taasisi mbalimbali iliyoandaliwa na Eagle Intertaiment award 2023.
Amesema lengo ni kuona vijana wakichangamkia fursa ,kuibua vibaji ,kufanya kazi kwa nguvu , kuleta mabadiriko na kuyafikia malengo ya serikali hivyo wataungana ili kufikia adhima hiyo
" Eagle Intertaiment inafanya kazi kubwa sana ya kusababisha vijana wanaingia katika ushindani ,kuimarisha ubora kwa wale walioshinda kwa kuwa ushindani huo ni wenye tija chachu ya utekelezaji wa ilani ya serikali na hamasa kwa jamii tutashirikiana pia tutatafuta na wadau wengine ili tuzo za mwaka ujao iwe zaidi ya leo " anaeleza.
Aidha Mkurugenzi wa Eagle Intertaiment Hassan Kuku anaeleza kuwa wamegusa kila aina ya kada kwa kutambua michango yao katika jamii na kampuni hiyo imekuwa ikiandaa tuzo hizo sasa ni mwaka wa tatu zilianza mwaka 2021 na waliziandaa kwa kiwango cha Wilaya yao lakini kwa mwaka huu zimekuwa na mafanikio kwa kiwango kikubwa yamefanyika kwa ngazi ya kimkoa.
Ameeleza kuwa tuzo hizo zimekuwa na mchango katika jamii kwani zimeweza kuibua watu wapya kila siku huku mtarajio ni kuwa mwakani watakuwa na kitu kikubwa zaidi , aliomba wadau,mashirika na kampuni mbalimbali kuwekeza katika tuzo hizo ili ziwe bora zaidi.
Naye Easter Baraka mshindi wa tuzo ya Mwandishi Bora wa habari za Mazingira anaeleza kuwa amepata hamasa zaidi ya kuibua na kuchakata habari zenye tija na zitakazoleta maendeleo kwenye jamii pasipo kutanguliza maslahi mbele.









