Rombo marathon, Ndafu Festival kufanyika Decemba 23

13Nov 2023
Anjela Mhando
ROMBO
Nipashe
Rombo marathon, Ndafu Festival kufanyika Decemba 23

MBUNGE wa Rombo mkoani Kilimanjaro, profesa Adolf Mkenda amewahimiza wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano ya kukimbia na kutembea ya Rombo Marathon na Ndafu Festival yaliyoandaliwa na ofisi ya mbunge kwa kushirikiana na taasisi ya michezo ya Wilaya hiyo,-

Mbunge wa Jimbo la Rombo Mkoa wa Kilimanjaro Profesa Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mashindano ya Rombo Marathano na Ndafu Festival yanayotarajiwa kufanyika December 23.2023.

-yanayotarajiwa kufanyika Desemba 23, 2023 katika eneo la Tarakea Rongai katika msitu wa wakala za wa huduma za misitu (TFS)

Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mashindano hayo yatafanyika kwa malengo, na tayari wameomba wadhamini baadhi kuwafadhili ambapo kiasi kidogo cha fedha hizo zitasidia katika maandalizi ya Marathon na kila mtu atachangia fedha, ambapo fedha nyingine zitatumika katika ujenzi wa vyoo bora katika shule za msingi na sekondari, pamoja na fedha nyingine zitakazopatikana zitaenda kusaidia harakati za kupanua hospitali ya huruma iliyopo Mkuu Rombo ili iweze kuwa ni hospitali ya kiwango cha Mkoa .

Mratibu wa mbio hizo, Temistocresi Isdori amesema eneo hilo la hifadhi ya msitu ambapo mbio hizo zitafanyika ni eneo lenye mandhari nzuri ya kuvutia, ikiwemo wanyama wadogo wadogo, miti na msitu mzuri ambapo ni wakuvutia,ambapo amesema washindi wa mashindano hayo watapata zawadi mbalimbali huku washiriki 1000, wakitarajiwa kushiriki, ambapo mbio hizo zitakuwa ni km 21,km 10, pamoja na km 5.

Hata hivyo amesema washindi wa mashindano hayo watapata zawadi mbalimbali huku washiriki 1000 wakidhaniwa kishiriki.

Katika mashindano ya mbio hizo kila mshiriki anapaswa kuchangia fedha kiasi cha shilingi 35,000, ambapo ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha, huduma za kwanza pamoja na watu wa msalaba mwekundu watakuwepo, huku wasanii mbalimbali wakishiriki mbio hizo.