Okwi aliuzwa na Simba Klabu ya Etoile du Sahel, lakini tangu wakati huo fedha za mauzo za mchezaji huyo hazikulipwa na kuibua maswali mengi kuliko majibu wakati wa utawala wa Rage.
Hata hivyo, klabu hiyo ya Tunisia imelipa fedha hizo kiasi cha Sh. milioni 600 baada ya kuamriwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Akizungumza jana, Rage alisema waliokuwa wakimtuhumu kula hela hizo za mauzo wa Okwi sasa wameujua ukweli.
Katika fedha hizo, Simba imepata nyongeza ya dola 19,000 kama riba ya fedha hizo kuchelewa kutumwa. Msemaji Simba, Haji Manara alikiri jana fedha hizo kulipwa na kusema kuwa uongozi utatoa ufafanuzi zaidi wiki ijayo.










