Pluijm: Al Ahly wanafungika kwao

12Apr 2016
Faustine Feliciane
Dar
Nipashe
Pluijm: Al Ahly wanafungika kwao

KOCHA wa Yanga, Hans van de Pluijm amesema kikosi chake kina nafasi ya kusonga mbele pamoja na kulazimishwa sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri katika mechi ya kwanza – raundi ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hans van de Pluijm.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Pluijm alisema anafahamu ugumu wa mashindano hayo, lakini anakiandaa kikosi chake kusonga mbele. "Sare hii siyo nzuri kwetu, lakini hatuvunji moyo kwenye mechi ya marudiano.

Bado tuna nafasi ya kusonga mbele,” alisema Pluijm.

Sare hiyo inatafsiriwa na mashabiki kama ndiyo mwisho wa Yanga kwenye mashindano hayo kutoka na ukweli kuwa timu za Tanzania hazina bahati zinapokwenda kucheza ugenini dhidi ya timu za Waarabu.

"Tunaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono, waondoe hofu kwa sababu bado tuna nafasi ya kufanya vziuri kwenye mechi ya marudiano,” alisema Pluijm.

Alisema kikosi chake kitaondoka mapema kwenye Misri ili kuzoea hali ya hewa kabla ya mechi ya marudiano. Ili kusonga mbele, Yanga inahitaji kushinda mchezo huo utakaopigwa ndani ya wiki moja na nusu ijayo nchini Misri.