Nyota hao waliukosa mchezo wa awali wa ushindi wa magoli 2-0 nyumbani dhidi ya timu hiyo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano walizopata katika michezo miwili mfululizo dhidi ya Al Ahly kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika.
Kocha wa Yanga, Pluijm alisema uwepo wa nyota hao kutawachanganya wapinzani wao ambao hawajawaona wakicheza.
"Uwepo wao utaongeza kitu ukilinginisha na mchezo wetu wa kwanza, tumekuja hapa kupambana na hatujaja kulinda ushindi wetu tulioupata nyumbani, hawajawaona Ngoma na Kamusoko wakicheza na hii ni faida kwetu," alisema Pluijm.
Aidha, alisema kuwa pamoja kuwa wapo mbele kwa magoli 2-0, watacheza kwa tahadhari kubwa kwenye mchezo huo wa leo utakaoanza saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
"Hatutajilinda tu muda wote wa mchezo, tutahakikisha tunakuwa makini kuwazuia wasipate goli na sisi tutapanga mashambulizi na kuhakikisha tunatumia vizuri kila nafasi tutakayoipata,' alisema Pluijm.
Kikosi hicho cha Yanga kilitua salama mjini Dundo kikitokea jijini Luanda kilipotua kikitokea Dar es Salaa mbapo kilitumia muda wa masaa mawili kwa ndege kutoka Luanda kuelekea Dundo utakapofanyika mchezo wa leo.
Mabingwa hao wa Tanzania bara, wanahitaji sare tu ili kuweza kusonga mbele na kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo inayoshika nafasi ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu Afrika baada ya magoli mawili ya Simon Msuva na Anthony Matheo kwenye mchezo wa awali kuipa utangulizi huo w amagoli 2-0.
Yanga imeingia kwenye michuano hiyo baada ya kutolewa hatua ya 16 bora ya klabu bingwa Afrika ilipoondolewa kwa jumla ya magoli 3-2 na Alh Ahly ya Misri baada ya awali kutoka sare ya goli 1-1 hapa nyumbani kabla ya kufungwa 2-1 ugenini.










