Felix alikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na matatizo ya kifamilia na leo anatarajiwa kuungana na kikosi kitakachoikabili Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
Mshambuliaji huyo aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kumaliza matatizo yaliyokuwa yanamkabili, ameeleza nguvu na akili katika kuifungia timu yake na kujinasua kwenye janga la kushuka daraja.
"Tuko kwenye nafasi ya 10 katika msimamo, haitakuwa nafasi yetu wakati ligi itakapofika mwisho, tutapambana kuhakikisha tubakaki kwenye ligi na nimerudi na shauku ya kuisaidia timu yangu," alisema Felix.
Hata hivyo nyota huyo alisema suala la kumpanga kikosini liko chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Mmalawi, Kinnah Phiri.










