Liewig aliiambia Lete RAHA kuwa Simba haiwezi kuifunga Stand kwa idadi kubwa ya mabao kama watu wanavyodhani.
“Sisi ndiyo tutakaotibua mipango ya Simba. Tutahakikisha tunawafunga na kuwamalizia kasi waliyonayo. Kuanza kwa rekodi ya kufunga goli moja na kuongeza idadi ya mabao kila inapocheza si kigezo kwani mpira si maneno.
“Ninaiandaa timu yangu kwa ajili ya kuwafunga Simba na nina imani nitawafunga, hivyo wasitegemee mteremko wowote tutakapokutana,” alisema kocha huyo ambaye aliwahi kuifundisha Simba miaka ya nyuma.
Mzungu Stand: Eti Simba wanipige 7, acheni utani
07Feb 2016
Lete Raha
Mzungu Stand: Eti Simba wanipige 7, acheni utani
HUKU kikosi cha Simba chini ya kocha Jackson Mayanja kikionekana tishio siku baada ya siku, kocha wa Stand United, Mfaransa Patrick Liewig, amesema ongezeko la idadi ya mabao ambayo Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakifunga katika kila mechi si kigezo cha kuifunga Stand magoli 7.










