Mtibwa walikumbana na kipigo hicho juzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Maxime alisema kipigo hicho hakukitegemea kutokana na maandalizi ya timu yake.
"Kwa sasa akili zetu tunazielekeza kwenye michezo yetu ya ligi kuu, nimehuzunishwa kutolewewa Kombe la FA, lakini ndio mpira ulivyo," alisema Maxime.
Alisema katika mchezo wa juzi, wenyeji wao Coastal Union walikuwa na bahati ya kupata ushindi.
"Tulijitahidi kuhakikisha tunawabana wapinzani wetu na kuibuka na ushindi, lakini wenzetu walikuwa na bahati ya mchezo," aliongezea.
Timu hizo zinatarajiwa kukutana tena Machi 5 kwenye mchezo wa ligi kuu, huku Mtibwa wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani, Manungu.
Coastal pamoja na Ndanda FC walioibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu juzi kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, wameungana na Yanga kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.










