Msichague viongozi wanaoishi Dar - Nape

07Apr 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Msichague viongozi wanaoishi Dar - Nape

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewataka wadau wa michezo nchini kutowachagua viongozi wa vyama mbalimbali wanaoishi Dar es Salaam na si mkoa ambao anauongoza.

Nape Nnauye.

Nape alisema hao juzi akiwa mkoani Kigoma na kueleza kwamba hali hiyo inawafanya viongozi hao kushindwa kuwatumikia vyema wananchi waliowachagua kwa sababu ya kutokuwa nao karibu.

Alisema kiongozi anayeishi Dar es Salaam utendaji wake hauwezi kufanana na kiongozi anayeishi eneo husika.
"Msiwachague viongozi wanaokaa Dar es Salaam, wao mnawaona wakati wa uchaguzi tu, muda mwingi wanakuwa nje ya mkoa," alisema na kuongeza:

"Hii haiwasaidii, wao wanaonekana wakati wa uchaguzi halafu wakishinda wanaondoka mpaka uchaguzi ujao," alisema Nnauye.

Alisema serikali inawaomba viongozi wote mikoani kufuata katiba zao na kutekeleza kalenda walizozipanga ili kuiendeleza michezo kuanzia ngazi ya wilaya.