Mayele amepachika mabao 15 wakati Ngoyi wa Ngoyi anayeitumikia Kitayosce ya Tabora ameshafunga magoli 13 mpaka sasa.
Kitayosce iko katika nafasi ya pili kwenye msimamo lakini nafasi ya pili katika ufungaji inafuatiwa na straika Mtanzania anayeichezea JKT Tanzania, vinara wa ligi hiyo amefunga mabao 11.
Adam Uledi wa Kengold FC anafuatia akiwa na mabao nane na Deogratius Kulwa anayeichezea Pamba FC, akifunga mabao saba.
Wachezaji waliofunga mabao sita kila mmoja ni Emmanuel Mpuka wa Kengold FC, Eliya Ashley (JKT Tanzania), Francis Ndala (Copco), Jeremiah Joseph na John Elius wote wa Mashujaa.
JKT Tanzania inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 53, ikifuatiwa na Kitayosce yenye pointi 46, Pamba FC nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na Mashujaa inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi 38 huku Fountain Gate iliyopo nafasi ya tano imejikusanyia pointi 37.
Mbeya Kwanza ya Mbeya iko katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 34, na tayari timu zote zimeshacheza michezo 22.
Timu mbili zitakazomaliza nafasi ya kwanza zitapanda daraja moja kwa moja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.










