Meja huyo mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aiinoa timu hiyo ya Mtwara msimu uliopita akirithi mikoba ya Dennis Kitambi kabla ya kutua City msimu kuchukua kiti cha Juma Mwambusi, lakini timu hiyo ya Mbeya iliamua kuachana naye na kumwajiri Mmalawi Kinnah Phiri baada ya kuwa na mwenendo mbovu Ligi Kuu.
Mingange aliiambia Nipashe jana kuwa ameanza mazungumzo na uongozi wa Ndanda FC na wako katika hatua nzuri.
"Nikweli Ndanda wananihitaji ili nikaongeze nguvu katika kikosi chao, naimani tutafikia makubaliano," alisema.
"Mimi sichagui timu ya kufundisha, timu yoyote itakanihitaji, niko tayari kufanya nayo kazi. Ligi ya safari hii ni ngumu sana kwa sababu timu zinapisha kwa pointi chache tu."










