Mgosi awa kocha msaidizi Simba

03Apr 2016
Dar
Lete Raha
Mgosi awa kocha msaidizi Simba

KOCHA Mkuu wa Simba Jackson Mayanja amesema Nahodha wa timu hiyo Mussa Hassan Mgosi ni kama msaidizi wake katika kikosi chake, kutokana na kawaida ya kumwachia kusimamia mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa kucheza mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Mussa Hassan Mgosi.

Simba iko mjini Dar es Salaam,chini ya kocha Mayanja ikiendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la TFF, kama Azam Sports Federaation Cup wiki ijayo.

Akizungumza na Lete Raha jana,Mayanja amesema kwamba amemchagua Mgosi kumsaidia katika kazi za uwanjani, huku yeye akiendelea na programu nyingine za maandalizi ya mazoezi ya kila sikukwa sababu ananidhamu tofauti na baadhi ya wachezaji wengine.

Mayanja amemsifu Mgosi kwamba ni muelewa kwa kile anachoambiwa na amekuwa akiwasimamia vizuri wachezaji wenzake kila anapokabidhiwa jukumu hilo.

Alisema kutokana na hilo, ana kila sababu ya kumchagua Mgosi kusimamia mazoezi ya timu hiyo akiwa kama Nahodha, na msaidizi wake wanapokuwa uwanjani kupasha kujiandaa na mechi mbalimbali za Ligi Kuu ya Bara.

Akizungumzia kwa upande wa maandalizi ya mchezo huo, alisema yanaendelea vizuri chini ya usimamizi wake ili kuhakikisha wanashinda katika Mmchezo huo na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

"Timu inaendelea kujifua kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo,tunahitaji kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo,"alisema Mayanja.

Alisema lengo lake ni kuona Simba inasonga mbele katika michuano ya kimataifa, baada ya kuikosa kwa muda mrefu sasa.