Mkuu wa Kitengo cha Utabibu wa City, Joshua Kaseko, alisema jana kuwa wachezaji wote 18 waliosafiri kutoka Mbeya hadi Tanga wako tayari kwa mechi hiyo ya raundi ya 23.
“Joseph Mahundi alipata majeraha kwenye mchezo uliopita (dhidi ya Stand United). Sasa yuko vizuri na tunatarajia atakuwa sehemu ya kikosi hapo kesho (leo)," alisema.
Kocha mkuu wa City (Phiri), alisema jana kuwa hali ya hewa ya jiji la Tanga si rafiki kwa nyota wake waliozoea baridi la Mbeya, lakini hataki kuifanya sababu kwa timu yake kupoteza pambano kabla ya kucheza.
“Hali ya hewa ya hapa ni tofauti sana na Mbeya, lakini hilo hatulitizami sana, tumejiandaa vya kutosha, asubuhi ya leo (jana) tumemaliza mazoezi na wachezaji wamepewa muda wa kuweka miili yao sawa kwa kuoga kwenye barafu, hakuna shaka yoyote kuwa tunazo pointi tatu hapa,” Phiri alikaririwa na mtandao rasmi wa City jana.










