Akizungumza jana, Mratibu wa mbio hizo, Camilius Wambura alisema kuwa maandalizi ya mbio hizo yamekamilisha na kueleza mshindi wa pili ataondoka na Sh. 650,000 wakati anayemaliza kwenye nafasi ya tatu atazawadiwa Sh. 400,000.
Wambura alisema pia kutakuwa na mbio za kilomita 10 na kilomita 2.5 kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 na zimelenga kuongeza hamasa kwa yosso hao kuupenda mchezo wa riadha.
"Tutakuwa na zawadi nyingine za kuanzia kwa wanariadha wanataoshika nafasi ya nne hadi ya 10," alisema mratibu huyo.
Aliongeza kuwa mbio nyingine zitakazoshindaniwa ni za umri mbalimbali pamoja na za baiskeli.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mbio hizo zitakazoanza na kumalizikia kwenye viwanja vya Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay.