Matokeo ya kupangwa, timu yafungwa 16-0

28Mar 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Matokeo ya kupangwa, timu yafungwa 16-0

WAKATI sakata la upangaji matokeo katika mechi za Ligi Daraja la Kwanza likiwa halijamalizika, kumetokea kisanga kingine cha Stand FC iliyokuwa inawania ubingwa wa mkoa Katavi kushinda mabao 16-0 dhidi ya Kazima FC.

Rais wa TTF Jamal Malinzi

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halijakubaliana na matokeo hayo na kuagizaa Chama cha Soka cha Katavi (KRFA) kufanya uchunguzi ndani ya wiki moja.

Kabla ya mchezo huo wa mwisho, klabu ya Nyundo FC ilikua inangoza kwa kuwa na pointi 21 na magoli 24 ya kufunga, wakati Stand FC ilihitaji ushindi wa mabao 13 ili kuweza kuwa bingwa wa mkoa hali inayopelekea kuwepo kwa dalili za kupanga matokeo.

KRFA haitaruhusiwa kutangaza bingwa wa mkoa hadi uchunguzi utakapokamilika na TFF kujiridhisha.