Katika michezo ya 17 ya Bandari imeingia siku ya pili ikiwa inaendelea kufanyika katika Viwanja tofauti ikiwamo Uwanja wa Jamhuri na Chuo kikuu cha Kiislamu Morogoro.
Katika Michezo ya juzi, asubuhi kwa upande wa mpira wa Pete, Timu ya Bandari ya Dar es Salaam iligalagazwa kwa magoli 34 kwa 31 dhidi ya timu ya Shirika la Bandari Zanzibar – ZPC, huku timu ya TPA Makao Makuu ikipata ushindi wa magoli 35 kwa 20 mbele ya Bandari Mtwara.
Kwa upande wa mchezo wa Mpira wa Kikapu timu ya Bandari Mtwara ilipoteza vikapu 56 kwa 52 na TPA Makao Makuu wakipata ushindi wa vikapu 102 kwa 46 dhidi ya Bandari za Maziwa, huku kwenye mpira wa wavu timu ya Makao Makuu ikiwanyoosha seti mbili kwa bila dhidi ya timu ya Bandari za maziwa.









