Leicester yaweka rekodi mpya ya ubingwa Ulaya

04May 2016
The Guardian Reporter
Nipashe
Leicester yaweka rekodi mpya ya ubingwa Ulaya

SARE ya mabao 2-2 kati ya Tottenham Spurs dhidi ya Chelsea Jumatatu usiku, iliipa fursa Leicester City chini ya Kocha Claudio Ranieri kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Leicester city

Kila timu ikiwa imebakiza mechi mbili mkononi, Leicester wana pointi 77, wakifuatiwa na Spurs wenye pointi 70, Arsenal wenye 67 na Manchester City katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 64.

Leicester ilianza kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo ikipewa nafasi ndogo ya kushinda taji hilo. Katika watu 5,000, mtu mmoja tu ndiyo aliipa nafasi ya kutwaa ubingwa timu hiyo iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita.

Lakini imeshinda taji hilo ikiwa imepoteza mechi tatu za ligi hiyo, huku ikiweka rekodi ya kuwa na kikosi kilichoonyesha ushirikiano wa hali ya juu.

Timu zilizokuwa zinawapa changamoto ni Spurs, Arsenal, Manchester City, Manchester United na waliokuwa mabingwa watetezi Chelsea, ambao walishindwa kutetea ubingwa wao kutokana na kasi waliyokuwa nayo mabingwa hao wapya maarufu kwa jina la 'Foxes'.

Mshambuliaji wa zamani wa Leicester, Everton na timu ya Taifa ya England Gary Lineker alieleza ubingwa wa timu yake ya zamani kama: "Ni mshtuko mkubwa katika ulimwengu wa michezo kuwahi kushuhudia katika maisha yangu".

Mtangazaji wa mechi mojawapo wa ligi hiyo aliiambia BBC michezo mwezi uliopita kuwa: "Siwezi kufikiria chochote kuhusiana na walivyopania kuweka rekodi. Ni ngumu kueleza kwa maneno.

"Nimefadhaishwa. Ilikuwa ni vigumu kutarajia. Nilikuwa ni kati ya watu tunaonunua tiketi za msimu tangu nikiwa. Hiki kilichotokea hakikuwezekana."

TAJI LA KWANZA KUBWA

Ubingwa wa England ndio taji kubwa kwa klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara wa Thai Vichai Srivaddhanaprabha na pia wamekata tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa Ulaya kuanzia hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.

Foxes walianza ligi huku wengi wakiiona kama timu dhaifu na itakayoshuka daraja sambamba na Watford, Norwich na Bournemouth.

Ranieri, ambaye alitua klabu hiyo baada ya kutimuliwa Nigel Pearson wakati wa majira ya kiangazi, alionekana si chaguo sahihi kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na mwenendo mbovu wa klabu yao iliyoshinda mechi saba za mwisho kati ya michezo yake tisa na kuifanya isiwe moja timu zilizoshuka daraja katika msimu mwaka 2014/15.

YAIJIBU BLACKBURN ROVERS

Tangu Ligi Kuu England ilipoanzishwa 1992/93, Blackburn Rovers peke yake ndiyo iliyofanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ukiondoa Manchester United, Arsenal, Chelsea au Manchester City.

Mara ya mwisho Leicester kumaliza ikiwa katika nafasi ya juu ilikuwa ni msimu wa 1928/29 na ilimaliza ligi hiyo ikishika nafasi ya pili na kukosa kutwaa taji kwa tofauti ya pointi moja.

Ranieri ambaye jina lake maarufu England, 'The Tinkerman' alifanya mabadiliko 27 katika kikosi chake msimu huu, huku akifanya mabadiliko mengi katika mechi dhidi ya Bournemouth.

Asilimia 42.3 Leicester imetwaa ubingwa ikiwa imecheza kwa kiwango cha chini katika kumiliki mpira tofauti na klabu nyingine zilizowahi kutwaa ubingwa huo tangu msimu wa 2006/07.

Kati ya mechi 22 walizoshinda Leicester msimu huu, haikucheza katika kiwango cha juu katika michezo 19 ukilinganisha na wapinzani wao.

Mapema Aprili, Leicester ilikuwa inaongoza kwenye msimamo ikiwa na tofauti ya pointi saba idadi sawa ya pointi walizotofautiana na timu iliyokuwa kwenye mstari wa kushuka daraja.

MECHI ZILIZOISAFISHIA NJIA

Leicester 3 Aston Villa 2, Septemba 2015: Mabingwa hao wapya walipata ushindi katika mechi hiyo dakika 18 za mwisho na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Stoke 2 Leicester 2, Septemba 2015: Ikitokea nyuma ilifanikiwa kusawazisha mabao hayo na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi.

Leicester 1 Manchester United 1, Novemba 2015: Straika Jamie Vardy alifunga bao lake la 11 msimu huu mfululizo na kuweka rekodi mpya kwenye ligi hiyo.

Leicester 2 Chelsea 1, Desemba 2015: Matokeo hayo yaliwafanya mabingwa watetezi Chelsea kukaribia kwenye mstari wa kushuka daraja, huku Leicester ikipanda kileleni.

Tottenham 0 Leicester 1, Januari 2016: Bao la kichwa la dakika za lala salama lililofungwa na Robert Huth liliwapoteza wapinzani wao Spurs katika mbio hizo za ubingwa.

Manchester City 1 Leicester 3, Februari 2016: Manchester City ambao nao walikuwa wanaufukuzia ubingwa huo, huku Riyad Mahrez akiwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli (14) kutoa pasi 10 za mabao.

Leicester 1 Southampton 0, Aprili 2016: Ulikuwa ni ushindi watano mfululizo kati ya mechi sita na kuwaweka kwenye nafasi nzuri huku ikiwa na mechi sita mkononi.

Leicester 4 Swansea 0, Aprili 2016: Licha ya straika wake tegemeo Jamie Vardy kufungiwa, Leicester hawakuonyesha hofu na hatimaye walipata ushindi huo mnono.