Phiri aliliambia gazeti hili kuwa alikuwa na uhakika wa ushindi kwenye mchezo huo na kusema kipigo hicho kimewavunja moyo.
“Tulijiandaa kushinda, ulikuwa mchezo muhimu kushinda kwa sababu ushindi ungetuweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi,” alisema Phiri.
Aidha, Phiri alimsifu mwamuzi aliyechezesha mechi hiyo, Israel Nkongo kuwa alicheza mechi kwa haki tofauti na malalamiko mengi dhidi ya waamuzi.
“Mwamuzi alikuwa bora, hakuna shaka kwenye ushindi wa Mtibwa Sugar, tulifanya kosa wakatuadhibu,” alisema.
Kuhusu mchezo ujao dhidi ya Yanga, kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi alisema anafahamu ugumu wa mchezo, lakini ana uhakika wa kucheza uwanja wa nyumbani kutampa ushindi.
“Kucheza dhidi ya Yanga kunahitaji maandalizi, tumerejea Mbeya mapema kwa ajili ya mechi hiyo na nina imani tutashinda.”
Katika mchezo huo wa juzi, goli la dakika ya 41 la Hussein Jvu lilitosha kuipa ushindi Mtibwa Sugar.










