Kikwete akutana na wanariadha Gabriel Geay na Wance Tarimo Boston

19Apr 2023
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kikwete akutana na wanariadha Gabriel Geay na Wance Tarimo Boston

Rais Mstaafu Dk.Jakaya Kikwete, amekutana na wanaridha Gabriel Geay na Wence Tarimo walioshiriki katika Mashindano ya Marathon yaliyofanyika Bostan, Marekani Aprili 17,2023.

Gabriel Geay aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo. JK, amempongeza Geay kwa ushindi mkubwa na kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Pamoja na wanariadha hao, walikuwepo pia wahamasishaji mbalimbali akiwemo 'Bongo Zozo' ambao wamepongezwa pia kwa kuhamasisha ushindi huo na kufanikisha kuinua bendera ya Tanzania.

Kikwete yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Haryard Ministerial Leadership Program'.Katika mafunzo hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi wa Zanzibar, Saada Mkuya ameshriki.