Karate kukinukisha Dar Aprili 24

04Mar 2016
Dar
Nipashe
Karate kukinukisha Dar Aprili 24

MASHINDANO ya taifa ya mchezo wa karate yaliyoandaliwa na shirikisho la mchezo huo nchini (Skita), yamepangwa kufanyika Aprili 24 kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko.

Mashindano hayo yenye lengo la kuchagua timu ya taifa, yatashirikisha klabu kutoka mkoa wa Pwani, Dar es Salaam na Morogoro ambazo ni mwanachama hai wa Skita.

Rais wa shirikisho hilo, Philip Chikoko, alisema Dar es Salaam jana kuwa tayari klabu nane zinethibitisha kushiriki katika mashindano hayo.

Alizitaja klabu hizo ni Upendo, Dolthine, Amani, Elephant, Ukombozi, Tanzanian Leonard, Home Boys na Kilakale.
"Kabla ya kuanza kwa mshindano, kutakuwa na semina elekezi kwa viongozi wa klabu pamoja wachezaji ambayo itaanza Machi 6-13," Chikoko.