Beki huyo amieleza Lete Raha kwamba ameamua kufanya hivyo kwakuwa kwake mpira ni kazi na kupiga hatua kwenye kazi ni kitu kizuri hivyo hatosita kuondoka pale atakapopata nafasi ya majaribio au dili nje.
“Ninafuraha na kile Simba imenifanyia mpaka sasa, ilinitoa nyumbani Uganda na kunipa nafasi na sasa ninajivunia kwa kile ninachokifanya.
“Hapa si mwisho wangu wa kucheza, nataka kwenda nje kujaribu maisha mengine. Naamini kile ambacho nilitaka kufanya Tanzania nimekitimiza ingawa ubingwa wa Ligi bado lakini ninaishukuru Simba kwa kunilea vyema.
“Kinachonipa moyo ni kuwa Simba ni klabu ambayo imekuwa ikitoa nafasi kwa kila mchezaji kuonesha kile ilichonacho hivyo nitatumia uzoefu na nafasi waliyonipa kupata nafasi nje,” alisema beki huyo wa zamani wa University of Victoria FC.
Juuko ambaye ana miaka 26 kwasasa ameitumikia Simba kwa misimu miwili mfululuzi akiwa moja ya wachezaji wenye nafasi za kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.










